TICAD: Japan yaahidi Afrika msaada wa dola bilioni 30.........
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi dola bilioni 30 za kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika, pamoja na msaada kwa kipindi cha miaka 3 ijayo, kwa lengo la kuimarisha ukuaji na biashara barani Afrika.
Theluthi ya pesa hizo itatumika kufadhili miradi ya miundo mbinu.
Bwana Abe ametoa ahadi hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la maendeleo barani Afrika nchini Kenya.
Kwa mara ya kwanza kongamano la sita la kimataifa la Tokyo kuhusu maendeleo barani Afrika (TICAD-VI) limeandaliwa barani Afrika.
Kongamano hilo limevutia wajumbe 10,000 na marais zaidi ya thelathini kutoka nchi za afrika, ambapo Japan inajaribu kurejesha ushawishi wake wa awali, na masoko ya nje, ambayo yamenyakuliwa na Uchina.
No comments