Ads

Mwalimu ahukumiwa kwa ubadhirifu.......


Geita.Mahakama ya Hakimu Mkazi  Geita imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka miwili mwalimu wa Shule ya Sekondari Msalala, Henry Tagata kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya  Sh9 milioni.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya waendesha mashtaka wa Takukuru,  Kelvin Mrusuri akisaidiana na Agustino Mtaki, hakimu Ushindi Swalo alisema kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na waendesha mashtaka wa Takukuru umethibitisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa  alitenda kosa hilo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.