Hatimaye Kocha wa simba akubali mabadiliko
Kocha Patrick Aussems amekiri wazi kuwa uwanja wa Sheikh Abeid jijini Arusha, ulimfanya yeye na timu yake wabadili aina ya mchezo ili waweze kuendana na uwanja na kupata matokeo mazuri.
Aussems ameyasema hayo leo jioni, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao African Lyon na kuendelea kujiweka vizuri katika mbio za kutetea ubingwa wao.
"Muhimu zaidi tumepata alama tatu. Tulijua kwamba uwanja sio mzuri na hivyo tulibadili kidogo aina ya uchezaji wetu kwa kucheza mipira mirefu na tulifanikiwa kufanya hilo'', amesema Aussems.
Kwa upande mwingine Aussems ameeleza kuridhishwa na kiwango cha wachezaji aliowaanzisha leo kwenye kikosi baada ya kuwapumzisha nyota wake kadhaa akiwemo Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na Clatous Chama.
Baada ya ushindi wa leo, Simba sasa imefikisha pointi 42 ikisalia katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga yenye pointi 58 pamoja na Azam FC ambayo ina pointi 50. Simba imecheza mechi tatu mfululizo za ligi kuu bila kuruhusu bao.
Naye mshambuliaji wa Simba Adam Salamba ambaye amefunga bao moja, amesema uwepo wake Simba pamoja na wachezaji kama John Bocco ambaye amefunga mabao mawili leo, unamfanya ajifunze vitu vingi na ndio maana anatumia vizuri kila nafasi anayopata na ana amini utafika muda atapata nafasi zaidi.
No comments