Ads

Raia 53 wameuawa Syria katika shambulio la makombora ya Urusi

ATHARI YA MAKOMBORA SYRIAHaki miliki ya picha
Takriban raia 53 wameuawa katika shambulio la kombora la Urusi katika kijiji kilichopo mashariki mwa Syria Al-Shafah, kundi la uangalizi linasema.
Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu Syria lililo na makao yake Uingereza (SOHR) linasema 21 kati ya wanaoripotiwa kuuawa Jumapili ni watoto.
Kijiji hicho kipo Deir al-Zour, mojawapo ya majimbo ya mwisho ambako wangambo wa Islamic State wanendelea kudhibiti ardhi.
Awali SOHR lilisema watu 34 wameuawa katika makombora yaliolenga makaazi ya watu .
Lakini mkuu wa shirika hilo limeliambia shirika la habari la AFP kwamba sasa wanaamini idadi hiyo ipo juu zaidi.
"Idadi hiyo imeongezeka baada ya kuondolewa kifusi baada ya operesheni ya siku nzima ya uokozi," Rami Abdel Rahman amesema.
KOMBORAHaki miliki ya pichaS
Awali Urusi ilithibitisha kwamba walipuaji wasita wa mabomu ya masafa marefu walitekeleza mashambulio ya angani katika eneo hilo, lakini ikasema iliwalenga wanamgambo na ngome zao.
Urusi ni mshirika wa kariu wa rais wa Syria Bashar al-Assad katika vita vya muda mrefu vya kiraia nchini humo.
Mazungumzo ya amani yanayoungwamkono na Umoja wamataifa yanatarajiwa kuanza upya Geneva wiki ijayo, lakini awamu kadhaa za mazungumzo hayakufuwa dafu.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.