Ads

Kwa simba hii lazima utaipenda tuuuu!!!!





SIMBA imeanza mechi za Ligi Kuu Bara kwa kuweka rekodi tano za maana ambazo zimewashtua Yanga na huenda zikawachukua mechi kadhaa kujibu mapigo.
Kipigo cha mabao 7-0 ilichokitoa kwa Ruvu Shooting juzi Jumamosi, kimeifanya Simba kuongoza Ligi kwa kishindo huku ikiweka rekodi za maana.
Kwanza, Simba inakuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa zaidi katika mechi ya kwanza ya ligi katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita. Rekodi ya karibuni ilikuwa ikishikiliwa na Yanga ambayo iliifunga Ashanti United mabao 5-1 katika mechi ya ufunguzi ya msimu wa 2013/14.
Pia ushindi huo umeifanya Simba kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika mchezo mmoja ndani ya miaka 10 iliyopita. Ushindi mkubwa wa mwisho kwa Simba ulikuwa dhidi ya Majimaji kwa mabao 6-1, hiyo ilikuwa Novemba 2015.
Simba pia imekuwa timu pekee iliyoweza kufunga mabao zaidi ya mawili katika mechi za ufunguzi wa ligi msimu huu.
Ushindi huo umeifanya pia Simba kuvunja rekodi ya Yanga kuifunga Ruvu mabao mengi ambapo ilifanya hivyo mwaka 2014 ilipoifunga kwa idadi kama hiyo ya mabao. Hata hivyo Simba bado ina kazi nzito ya kuvunja rekodi ya mabao 8-0 ambayo Yanga inaishikilia kwa kuifunga Coastal Union mapema 2015.
OKWI NAYE
Emmanuel Okwi amevunja rekodi ya Mrundi, Amissi Tambwe ambaye ndiye mchezaji wa sasa aliyewahi kufunga mabao manne kwenye mchezo mmoja. Tambwe alifunga mabao manne wakati Simba ikiifunga Mgambo JKT kwa mabao 6-0 mwaka 2013 na Yanga ilipoifunga Coastal Union 8-0.
Okwi amefunga ‘Hat Trick’ yake ya pili tangu alipoanza kucheza ligi hiyo mwaka 2009 kabla ya kuondoka na kurejea mara mbili tofauti. Hat Trick yake nyingine alifunga dhidi ya Ndanda mwaka 2015.
Mabao hayo yamemfanya Okwi kuwa mchezaji aliyefunga hat Trick ya mapema zaidi Ligi Kuu ambapo alitumia dakika 32 tu kufanya hivyo wakati wachezaji wengine wote waliomtangulia walitumia dakika zaidi ya 45.
“Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wamedhamiria kufanya kitu kwenye ligi, tutapambana kwa nguvu kwa pamoja na kuipa mafanikio Simba,”alisema Okwi ambaye pamoja na kufunga mabao hayo manne na kuwa kinara kwenye safu ya ufungaji bora, amesema kazi bado.
Akizungumzia sababu ya kuuingiza mpira ndani ya jezi yake tumboni,  alisema: “Nimefanya hivyo kwa makusudi, mke wangu ni mjamzito na hii ilikuwa ni ishara ya zawadi kwake.”
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema: “Tunaendelea kufanya maboresho kwa kuimarisha safu ya ushambuliaji.”|
Katika mchezo huo, Mganda Okwi aling’ara baada ya kufunga mabao manne peke yake.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.