IGP Siro atoa mtaji wa biashara kwa jambazi sugu
Mkuu wa Polisi nchini Kamanda Simon Sirro amempa mtaji wa kufungulia duka la mitumba jambazi aliyekuwa tishio mjini Tanga kwa zaidi ya miaka 25 baada ya kuacha kazi hiyo.
Jambazi huyo anayefahamika kwa jina la Nuni Dunduu (Sirro mdogo) amewataka vijana wanaondelea kujihusisha na kazi hiyo waache mara moja .
Alisema baada ya kujisalimisha katika ofisi ya Kamanda huyo wa Polisi alimpatia mtaji na kwasasa ni mfanyabiashara wa mitumba katika soko la Mgandini .
‘’Mwaka 2009 wakati Sirro akiwa kamanda wa polisi mkoani hapa alinipatia kiasi cha Sh 50,000 kama mtaji wa biashara nikaanza kukaanga mihogo na baada ya kuona naumia kwa moshi nikaamua kuuza mitumba ambayo mpaka leo ndiyo kazi yangu’’alisema na kuongeza
“ Wakati nikiwa jambazi nilikuwa naishi kwa wasiwasi nikimuona hata mtu anakuja karibu yangu nilikuwa naogopa najua kanifuata mimi, hivyo kazi hiyo inakufanya uishi kwa uoga na kama mkimbizi kwani unakuwa huna imani na mtu yeyote” Alisema Nuni
Aidha alisema kuwa anamshukuru Sirro kwani yeye ni mtu ambaye amemfanya kwa sasa aweze kuishi maisha mazuri na huru kama raia wengine wa Tanzania pamoja na kumuwezesha kufanya biashara hiyo ambayo kwasasa inampatia kipato.
IGP sirro alithibitisha kumpokea ofisini kwake kijana huyo ambaye alikuwa jambazi sugu na kusema kwasasa wamekuwa marafiki wazuri na amekuwa mtiifu na mzalendo kwa nchi yake.
Sirro aliwataka majambazi wengine ambao bado wanaendelea na kazi hiyo waache kazi hiyo na wajisalmishe kama alivyojisalimisha Nuni ambaye alimpa jina la sirro mdogo , aliongeza kuwa mmemuona Sirro Mkubwa na Sirro Mdogo kwa sasa mtu huyu anaitwa Sirro mdogo.
Nuni alisema kilichomfanya aache ujambazi ni baada ya wenzake wengi kupoteza maisha huku wengine kufungwa jela jambo ambalo lilimfanya aishi kama mkimbizi ndani ya nchi yake.
‘Hizo ni sababu ambazo zilinifanya kwenda kujisalimisha mwenyewe kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga wakati huo alikwa ni Kamanda Simon Sirro ambaye ni IGP kwa sasa’’alisema
Akizungumzia Suala la Kibiti alisema kuwa Kibiti kwa sasa kuko shwari na aliwataka waandishi wa habari wawaeleze wakazi wa tanga wasiogope kwenda kibiti kwani kwasasa kuko shwari .
“ Nendeni Kibiti msiogope kwasasa kuko shwari watu wale wabaya wameshaondoka katika eneo la kibiti ’’ Alisema Sirro.
“ Naziomba zile kamati za ulinzi na usalama kuanzia ngazi zote za kijiji mpaka mkoa kufatilia habari za waharifu na kutoa taarifa kwa vyombo husika kwani watu hao sio wazuri wamebadilika wamekuwa wanyama na wanamuua mtu yeyote ambaye hajagombana na bila sababu ya msingi” Alisema IGP Sirro.
Akizungumzia suala la kukamatwa Wanasiasa alisema wao kama Jeshi la Polisi wanakamata watuhumiwa ambao wanaamini wamefanya makosa ya jinai lakini wakifanya upelelezi wakigundua mtuhumiwa hana kosa wanamuachia na . Tukina tuhuma ni za kweli tunampeleka mahakamani .
No comments