UGANDA,KABURI LA MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA LAFUKULIWA...
Kaburi la Mtunzi wa Wimbo wa Taifa wa Uganda marehemu George Kakoma limefukuliwa na watu wasio julikana, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mabaki ya mwili wake yameibiwa.
Gazeti la Daily Monitor la Uganda, limechapisha picha ya kile kilichoonekana kuchimbuliwa kaburi hilo na kuharibiwa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, polisi wa eneo hilo na mjane wa marehemu wameomba kibali mahakamani kuweza kuchimbua kaburi hilo, ili kuweza kuthibitisha kama mabaki yake yapo ama yameondolewa.
Marehemu Kakoma alifariki dunia miaka mitano iliyopita.
No comments