TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI JULY 16.2017
Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday)
Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport)
Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday)
Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror)
Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN)
Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Danny Rose, 27. (Sunday Express)
Stoke City wanasubiri West Ham kupanda dau la tatu kutaka kumsajili Marko Arnautovic, 28. Stoke wanataka pauni milioni 22.5. (Mail on Sunday)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23, atabakia Emirates, licha ya Liverpool kumtaka. (Metro)
Leicester City wanataka pauni milioni 40 kumuuza Riyad Mahrez, 26, kwenda Roma. Chelsea na Everton pia wanamtaka winga huyo. (Mail on Sunday)
Riyad Mahrez tayari amekubaliana na Roma. (Mediaset)
Beki wa kulia wa Real Madrid, Danilo, 26, anataka kuhamia Chelsea. (Diario Gol)
Manchester City nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 26, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 21.9. Chelsea na Juventus wanamtaka pia beki huyo kutoka Brazil. (Sunday Times)
Kiungo wa Manchester United Ander Herera, 27, atasaini mkataba mpya wa miaka minne wa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki kubakia Old Trafford. (Daily Star Sunday)
Andrea Belotti ameiambia AC Milan anataka kujiunga nao, lakini klabu yake, Torino inataka euro milioni 100. Milan wapo tayari kutoa euro milioni 40 pamoja na Gabriel Paletta na M'Baye Niang. (Calciomercato)
Everton wanapanga kutoa pauni milioni 30 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott. (Sunday People)
Winga wa Monaco, Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya Monaco kumruhusu kuondoka na kujiunga na Arsenal. (Daily Star).
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amekataa kuhamia Beijing Guoan. (Sunday People)
Ivan Perisic ameondoka katika kambi ya mazoezi ya Inter Milan, huku kukiwa na taarifa zaidi kumhusisha na kuhamia Manchester United. (Calciomercato)
Manchester United wanataka Real Madrid imhusishe Toni Kroos katika mkataba wowote wa kumtaka kipa David de Gea. (Daily Mirror)
AC Milan wanataka kumsajili Luka Modric, lakini watakabiliwa na kazi ngumu kumshawishi kiungo huyo kuhamia San Siro. (Calciomercato)
Barcelona wapo tayari kuongeza dau hadi euro milioni 30 kumsajili Paulinho kutoka Guangzhou Evergrande. (Mundo Deportivo)
Inter Milan wanataka kuwapiku Liverpool katika kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita. (Calciomercato)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.
No comments