Ads

SAFARI YA ABRI BANDA YAZUA UTATA MSIMBAZI


Image result for lion

Dar es Salaam. Baada ya beki Abdi Banda kuilalamikia klabu yake ya Simba kuwa inambania kutimkia Afrika Kusini kucheza soka ya kulipwa, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kumtaka beki huyo kufuata taratibu.
Banda alilalamika juzi kupitia vyombo vya habari kuwa viongozi wa Simba wanakwamisha mpango wake wa kujiunga na klabu ya  Baroka F.C ya Afrika Kusini baada ya kumnyima barua ya uthibitisho wa kumaliza mkataba.
Beki huyo alisema juzi alikwenda kuwaona viongozi wake ili  wampatie barua ya uthibitisho wa kumaliza mkataba wake, lakini viongozi wamekuwa wakimzungusha.
"Nishamaliza mkataba na Simba na niliwafuata viongozi wangu wanipe barua tu ya kuonyesha kuwa nimemaliza mkataba, lakini  nimeenda ofisini tangu asubuhi nazungushwa sasa siwaelewi kwani muda nilionao ni mchache na natakiwa nirudi Afrika Kusini wiki hii. Sitaki kuondoka ndani ya klabu hii vibaya kwani nimeishi nao vizuri lakini hiki wanachonifanyia kinanishangaza," alisema Banda.
Wakijibu shutuma hizo uongozi wa Simba leo Jumanne umetoa taarifa kwa vyombo vya habari, ilisema ni kweli mchezaji huyo amemaliza mkataba na klabu hiyo, lakini  wanashangaa mchezaji huyo kukimbilia katika vyombo vya habari  na kuipaka matope na kuishushia heshima klabu.
"Ni kweli Banda amemaliza mkataba na klabu na jana alikuja ofisini kwetu kutaka barua hiyo,lakini akakumbushwa  kuwa ukiwa umemaliza mkataba haupaswi kupewa barua hiyo ,wanaoandikiwa barua hiyo ni waajiriwa ambao bado wana mkataba na labda kwa sababu yoyote ile klabu itaamua kuachana nao.
"Lakini kwa kuwa Banda aliitaka hiyo barua akaambiwa aandike barua fupi tu ya kuomba barua ya uthibitisho ili ibaki kumbukumbu kwa klabu lakini kwa mshangao wa maafisa wa klabu aligoma kuiandikia barua klabu na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari"ilisema taarifa hiyo.
"Simba inaamini utamaduni wake wa miaka mingi wa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda nje ya nchi kucheza soka pindi  wapatapo nafasi hiyo lakini inasiistiza sana suala la utaratibu,haijawahi kutokea kokote duniani mchezaji aliyemaliza mkataba kudai barua ya uthibitisho.
"Kupitia barua hii klabu inawaambia haitafanya kazi kwa shinikizo la mtu au chombo chochote kile huku tukifahamu  ni kinyume na utaratibu na utamaduni wa mchezo huo unaopendwa duniani kote"ilieleza taarifa hiyo,
Taarifa hiyo ilisema kuwa Banda akitaka barua yao. ni wajibu wake kuandika barua pia vinginevyo wanamtakia mafanikio makubwa huko aendako.  

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.