Ads

MDEE AKAMATWA NA POLISI...

Image result for halima mdee

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay .


Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza na gazeti la  Mwananchi  jana  saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.

 Awali akizungumza na waandishi wa habari jana asubuhi,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo  kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya  hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.