Ads

MDEE ADAI MAPAMBANO YANAENDELEA




Image result for halima mdee



Baada ya kupata dhamana siku ya Juma tatu, kutokana na madai ya kutoa lugha chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee  amedai mapambano yake juu ya watoto wa kike kupata elimu bado yanaendelea.


Mdee ametoa kauli yake hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wakati akiwashukuru wananchi na wadau waliopaza sauti kwa kitendo cha yeye kuwekwa chini ya ulinzi kwa zaidi ya muda uliopangwa.

"Kwa heshima kubwa niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! Mapambano yanaendelea!" aliandika.

Halima Mdee aliwekwa chini ya ulinzi kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Happi kwa kuadai kwamba mbunge huyo alitoa maneno kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake CHADEMA uliofanyika katika ofisi za baraza hilo wakati akizungumza na wanahabari.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.