Ads

KOTEI AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI SIMBA


Image result for kotei simba

 Kiungo Mghana, James Kotei ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba hadi 2019, na kumaliza uvumi kuwa huenda angejiunga na watani zao Yanga.


Kotei alimaliza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mwezi uliopita, lakini mazungumzo ya kuongeza mkataba yalikwenda vizuri kabla ya kusaini mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Kotei alisema anajiandaa na kazi Msimbazi hasa baada ya kufanya vizuri katika miezi sita iliyopita ambapo alichezeshwa kama beki wa kati pamoja na kiungo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.