Ads

KAMUSOKO MAMBO SAFI JANGWANI


Image result for KAMUSOKO

Image result for advertise here

Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili.
Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya mambo kadhaa.
Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka huu nchini Gabon.
Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.