DALALI AJITOA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA
ar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ni mzoefu wa mechi za watani wa jadi nchini, baada ya kusikia ratiba ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Agosti 23, fasta ameibuka na kutoa la moyoni.
Dalali alisema pambano hilo la watani litakuwa kipimo tosha kwa Kamati za Usajili za klabu hizo kama wamesajili majembe au la.
Dalali ambaye katika miaka yake minne ya uongozi Simba alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu, alisema ni kawaida kwa mashabiki wa Simba na Yanga, kuanza kutambiana nyota wapya wanaoingia ndani ya vikosi vyao, kabla ya kuona uwezo wao uwanjani, hivyo Ngao ya Jamii itatoa picha halisi.
"Heshima ya kamati za usajili, zitaanza kuonekana Agosti 23 kwa maana wachezaji kucheza soka ni kazi yao, hawatakuwa na jambo la kusingizia," alisema.
Aliielezea mechi hiyo kwamba itatoa taswira ya wachezaji walipo ndani ya klabu hizo kwamba wana uwezo wa kiasi gani ambao utakuwa mfano kwa klabu nyingine.
"Wachezaji wanatakiwa kuelewa kwamba mechi ya Ngao ya Jamii, itawakuwa mtego kwao licha ya kwamba ni ya burudani na haina madhara yoyote, lakini kwa kuwa Simba na Yanga hawana dogo wajitathimini uwezo wao ili waaanze kujijengea heshima ya kuaminiwa na mashabiki wao,"alisema
Nahodha wa Simba, Jonas Mkude alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya kitu kitakachokuwa faraja kwa mashabiki wao.
No comments