ABRI BANDA, SIO SIMBA TENA SASA NI BOROKA FC MIAKA MITATU...
Aliyekuwa beki wa klabu ya Simba Abdi Banda amekubali kuweka wazi kuwa hatoendelea kuitumikia Simba SC msimu ujao kwani ameshajiunga na klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.
Banda alisema hayo baada tu ya kuwasili Tanzania akitokea Afrika Kusini alipokuwa akishiriki michuano ya COSAFA Cup akiwa na Taifa Stars.
Aidha mchezaji huyo amesema amekuja Tanzania kwa ajili ya kuaga kabla ya July 12 kurejea Afrika Kusini kuungana na timu yake mpya ya Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.
"Ni ishu ambayo imekuwa rasmi kwa sasa hivi lakini ya muda mrefu, kwa hiyo nimekuja tu nyumbani mara moja kupata baraka , nimekuja kuaga viongozi wangu wa zamani wa Simba ambao nimekuwa nao muda mrefu kisha niondoke rasmi” - Banda
Abdi Banda ni mchezaji wa tatu kuondoka katika klabu ya simba, mwingine ni Ibrahim Ajib aliyesajiliwa na klabu ya Yanga na Pastory Athanas aliyesajiliwa na klabu ya Singida United.
No comments