Wanasayansi wagundua sayari 10 zenye dalili za uhai...
Wataalam wa maswala ya angani wametangaza ugunduzi wa sayari nyengine kumi angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.
Wanasayansi wa shirika linaloshughulikia maswala ya angani NASA wanasema kuwa data mpya iliochunguzwa kutoka kwa darubini ya Kepler inaonyesha sayari kumi zenye miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.
- Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars
- Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa
- Unyevu katika sayari ilio sawa na dunia
- Jiwe kubwa lapita karibu na Dunia
Sayari hizo ambazo zinatoshana na dunia, zote zipo nje ya jua katika mkusanyiko huo wa nyota.
Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua jumla ya sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.
No comments