Uamuzi wa Trump kupinga baadhi ya raia wa kiislam kuhatarisha nchi....
Mwanasheria mkuu wa Marekani Jeff Sessions amesema pingamizi la kimahakama dhidi ya hatua ya rais Trump kupiga marufuku baadhi ya raia kutoka nchi za kiislamu kuingia Marekani mahakama kupinga hivi karibuni ni kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Idara ya sheria nchini humo iliahidi kupinga hatua hiyo ya rais Trump katika mahakama ya juu.
Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco,ni kufuatia umamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump,akisistiza kuwa kila lilalowezekana linatakiwa kufanywa kwaajili ya ulinzi wa Marekani
"nadhan wote tunafahamu kuwa hizi ni nyakati za hatari dhidi ya tishio la ugaidi,tunapaswa kuwa kulinda kuingia kwa watu wanaoweza kufanya vitendo vya ugaidi na uwagaji wa damu.Tunaendelea kuwa na Imani kwamba amri za rais wetu ni kwa mjibu sheria na kwamba tunaamini mahakama ya juu itazipitisha"
Hata hivyo mwanasheria mkuu wa jimbo la Maryland na Columbia Brian Frosh amefungua mashitaka dhidi ya rais Trump kwa madai ya kupokea malipo ya nje kupitia makampuni yake.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Frosh Mwana Maryland's Attorney Generel, Brian Frosh, ameseama Trump kujihusisha biashara akiwa madarakani ni kuvunja katiba
"Aliiteuwa Hoteli yake ya kimataifa ya Trump kwaajili ya wanadiplomasia na maofisa wa serikali. Amekuwa akionekana kwenye sehemu nyingi za biashara zake na imekuwa kama sehemu ya kutangaza biashara hizo.Analipwa na makampuni yanayo milikiwa na nchi za nje kama vile China ambao pia ni wapangaji katika majengo yake.Na amekuwa akiendelea kuchukua malipo kutoka nchi za Saudi Arabia, India, Afghanistan na Qatar nchi ambazo zina hisa majengo yake ya kibiashara yajulikanayo kama Trump World Tower.
Rais Trump amekuwa akikabiliwa na upinzani mkali kufuatia baadhi ya maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya tangu kuingia madarakani,ikiwemo hatua hii aliyoichukua kupiga marufuku raia kutoka baadhi ya nchi za Kiislam kuingia Marekani
No comments