Ads

Torino yazigomea AC Milan, Man United...



Milan, Italia. Klabu ya Torino imedhamiria kumzuia nyota Adrea Belotti ili abaki kikosini hapo kwa ajili ya kuisaidia timu yake msimu ujao.
Mshambuliaji huyo, alionyesha kiwango kizuri kwenye mechi za Seria A msimu wa 2016/17, huku akifunga mabao 28 jambo lililozivutia klabu mbalimbali barani Ulaya.
Naye, Rais wa klabu hiyo Urbano Cairo alisisitiza kwamba hakuna sababu ya kumuuza Belottti.
Mchezaji huyo mwenye miaka 23 amekuwa akihusishwa kujiunga na AC Milan pamoja na Manchester United.
Nguvu ya Jose Mourinho ameielekeza kwa mchezaji huyo baada ya kukwama kudaka saini ya mchezaji Alvaro Morata.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.