Lazima tujifunze kutoka kwa Gadafi......
Mwaka 1955 Libya iliingia mkataba wa kuchimba mafuta na kampuni ya Kimarekani iliyokuwa inaitwa 'Libyan American Oil Company' wakati huo Libya ikiwa chini ya Mfalme Idris. Baadaye Marehemu Muhammar Gaddafi akafanya mapinduzi na kuitawala Libya.
Muammar Gaddafi alikuta Libya ipo kwenye mikataba ya ajabu ya Mafuta na kampuni hiyo ya USA ambayo ilikuwa inanufaisha wazungu kuliko Libya na siku moja kwa hasira sana na uchungu wa kuona nchi yake inanyonywa kwa neno MKATABA alisema... "WANANCHI WA LIBYA WALIISHI MIAKA 5,000 BILA OIL HAKUKUWA NA TATIZO KWA HIYO WANAWEZA KUACHANA NA OIL MPAKA NITAKAPOREKEBISHA MIKATABA UPYA ILI WANUFAIKE NA MAFUTA YAO"
Muammar Gaddafi kwa ujeuri mkubwa akafanikiwa kubadilisha mikataba na kwa mara ya kwanza Libya ikaanza kuchukua 51% ya mapato ya mafuta yake kutoka 25% ya mikataba uchwara na akafanikiwa kutaifisha uchimbaji na utafutaji mafuta Libya kwa 100% ikawa chini ya Taifa lake.Libya ikawa Taifa la kwanza Duniani kufanikiwa kuwa na Majority Share ya Mafuta yake ingawa pia Mabadiliko hayo ya sheria yaliingiza Libya katika migogoro mkubwa sana na Kampuni ya Libyan American Oil Company kiasi cha kufungua kesi dhidi ya Libya kama nchi na baadaye Libya kulazimishwa kuilipa kampuni hiyo pesa nyingi na mahakama ya Dunia.
Bado Muammar Gaddafi hakujali alisema.... "HATA TUKIWALIPA MAPATO YOTE TUNAYOYAPATA LAKINI CHA MSINGI NI PESA YA MAFUTA YETU SIO YAO KAMA ILIVYOKUWA"
Baadaye Libya ilifanikiwa kumaliza deni na kuwa Taifa la kwanza Afrika kufanikiwa kuwa na Social Security ya kuwatunza wazee wote nchini humo.
Leo Tanzania miaka 55 ya uhuru bado tunahangaika na wachimba madini yetu, leo Rais Magufuli anataka tuanze kufikiria kama Muammar Gaddafi kuna wanaopinga na kutaka tuendelee kuwalamba miguu Wazungu. Hapana tunaweza kufanya aliyoyafanya Muammar Gaddafi. Yaani Tunaweza kuchimba madini yetu kama tutaachana na Dollar na kununua 'TECHNOLOGY' ya kuchimba madini yetu wenyewe.
Rais Magufuli kanyaga twende, asiyetaka akae pembeni! ..
No comments