Kwahili lazima ukubali kweli Bongo bahati mbaya....
kila safari inakuwa na mwisho wake na hili limejidhihirisha leo, unajua sio kuwa hawawezi ila kuna kuzidiana na mdomana tunasema kweli bongo bahati mbaya.Wengi walitarajia kuwa itakuwa sifa kubwa kwa tanzania kuwakaribisha Everton kwenye nchi yao lakini mambo hayajaenda kama walivyodhinia.
Juzi jumanne walianza kutoka wale wa mchangani tukawa namatumaini kuwa huwenda wale wa jangwani watafanikiwa kutubebea zile milioni sita ila wakenya wakasema hapana hata sisi tunazitaka na leo wameamua kuwatangazia watanzania kuwa kweli Bongo bahati mbaya.
Leo ilikuwa ni mchezo wa nusu fainali ya kombe lililoandaliwa na kampuni inayojihusisha na mambo ya mpira (Sport pesa) kati ya Mabingwa wa lihi kuu Tanzania bara Yanga Fc na timu kutoka kenya AFC leopard ambapo timu hiyo kutoka Kenya imefanikiwa kuingia fainali kwa kuwatoa Yanga kwa mikwaju ya penalt.
Tanzania ilishirikisha timu nne ambazo ni Simba,Yanga,Singida Untd na Jang'ombe zote zimetolewa, na Kenya nao walishirikisha timu nne ambapo ni Tusker, Nakuru all stars, AFC Leopards na Gormahia zimetoka mbili na fainali zimeingia mbili.
Muda mwingine ukweli unauma ila kwahili lazima tukubali kuwa kweli bono bahati mbaya
By Ally mshana
No comments