Ads

Rasta wa Simba noma sana...


Image result for rasta wa simba
SIMBA juzi Jumanne iling’olewa katika michuano ya Kombe la Sport Pesa kwa penalti na timu ya Daraja la Kwanza ya Kenya, Nakuru All Stars, lakini mashabiki wa timu hiyo walionekana kuridhika na uwezo wa bekiwao mpya, Jamal Mwambeleko kwa namna alivyopiga mpira mwingi Uwanja wa Uhuru.
Beki huyo wa kushoto aliyecheza kwa dakika zote 90 na kuipa Simba matokeo ya 0-0, alionyesha wazi mfumo wa klabu hiyo ni rahisi kwao licha ya kuichezea kwa mara ya kwanza akitokea Mbao FC.
Mwambeleko anayefahamika kama Rasta, katika dakika hizo 90 Mwanaspoti ilimfuatilia na kubaini aligusa mpira mara 80 na kupiga jumla ya pasi zilizofikia kwa walengwa mara 60, zisizofika zikiwa tano na krosi tatu.
Pia alipiga tackling mara mbili, na kulenga lango kwa shuti moja, huku akipokonywa mipira mara tatu kati ya sita aliyopokonya yeye kwa Wakenya. Akizungumza na Mwanaspoti, beki huyo alisema hawezi kupata tabu Simba kwa sababu mfumo inayotumia ni wa kisasa na rahisi kwake kuumudu. “Mfumo wa aina hiyo ni mzuri kwasababu unanifanya kucheza kwa kufurahia mpira maana unanihitaji muda mwingi kupanda na kusaidia mashambulizi na kurudi haraka kuzuia wakati tunapokuwa hatuna mpira.
“Niko fiti kimazoezi ndio maana niliweza kumudu kucheza staili hiyo,” alisema Mwalembeko aliyekuwa akishangiliwa.     
mwanaspoti..

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.