Ads

Azam yamnasa Hoza kiumafia.....





Dar es Salaam. Klabu ya Azam imefanikiwa kumnasa kiungo wa Mbao FC,  Salmin Hoza aliyekuwa akiwaniwa na Yanga.
Hoza amesaini mkataba wa miaka miwili Azam muda mfupi baada ya kurudisha Sh 5milioni alizopewa na Yanga awali.
Hoza amefurahia kusaini Azam na kuahidi kuonyesha kiwango bora ndani ya timu hiyo yenye maskani yake Chamazi.
 "Mambo yalikuwa juu juu sana maana nilistuka wakati tayari watu wa Yanga wapo na walikuwa tayari tupo kwenye mazungumzo nao, mara wakaja na Azam, nilichokifanya nikitizama wapi wanamzigo.
"Yanga hawakuwa na mzigo kamili mkononi hivyo niliona ni bora kusaini kwenye timu ambayo imekuja na mzigo kamili, nimefurahi kujiunga na Azam ni moja ya timu kubwa nchini hivyo nitajitahidi kuendelea kuonyesha kiwango bora ndani ya timu hiyo" alisema Hoza.
Kutua Hoza anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam baada ya kumnasa Waziri Junior kutoka Toto Africans.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.