Salomon Kalou arejea kikosi cha taifa Ivory Coast...............
Mkufunzi mpya wa Ivory Coast Marc Wilmots amefanikiwa kumshawishi aliyekwua mchezaji wa Chelsea Salomon Kalou arudi kuchezea timu ya taifa.
Mchezaji huyo ametajwa katika kikosi cha wachezaji 27 watakaochezea timu hiyo ya taifa.
Kalou, ambaye amekuwa akichezea Hertha Berlin, alistaafu baada ya ndovu hao kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.
Kalou, 31, alikuwa ametangaza michuano hiyo ya Gabon ingekuwa yake ya mwisho lakini kwamba alikuwa anafikiria uwezekano wake kuchezea Ivory Coast hadi Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Wilmot pia amefanikiwa kuwashawishi wachezaji wanne waliochezea timu ya vijana ya taifa la Ufaransa kubadili msimamo na kuamua kuchezea Ivory Coast.
Jean-Philippe Gbamin, Jeremie Boga na Maxwell Cornet wanaweza wakachezeshwa mara ya kwanza Juni. Seko Fofana anauguza jeraha.
Ivory Coast watakutana na Uholanzi mechi ya kirafiki Juni 4 na dhidi ya Guinea siku tano baadaye mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika.Mechi hizo zitakuwa za kwanza za Wilmots tangu kuteuliwa kwake Machi.
Wachezaji nyota kama vile Didier Drogba, Didier Zokora, Kolo na Yaya Toure walistaafu soka ya kimataifa karibuni.
Kikosi cha Ivory Coast:
Walinda lango: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe, DR Congo) Axel Kacou (Tours, Ufaransa), Mandé Sayouba (Stabaek, Norway), Ali Badra Sangaré (AS Tanda, Ivory Coast), Abdoul Karim Cissé (SC Gagnoa, Ivory Coast)
Mabeki: Serge Aurier (Paris St Germain, Ufaransa), Mamadou Bagayoko (St Truiden, Ubelgiji), Eric Bailly (Man Utd, England), Simon Deli (Slavia Prague, Jamhuri ya Czech), Lamine Koné (Sunderland, England), Ismaël Traoré (Angers, Ufaransa), Wilfried Kanon (ADO Hague, Uholanzi), Adama Traoré (FC Bâsel, Uswizi), Joris Gnagnon (Rennes, Ufaransa), Ghislain Konan (Guimaraes, Portugal)
Viungo wa kati: Cheick Doukouré (Metz, Ufaransa), Franck Kessié (Atalanta, Italia), Geoffroy Serey Dié (FC Basel, Uswizi), Jean-Philippe Gbamin (Mainz, Ujerumani), Jean Michaël Séri (Nice, Ufaransa)
Washambuliaji: Nicolas Pépé (Angers, Ufaransa), Maxwell Cornet (Lyon, Ufaransa), Giovanni Sio (Rennes, Ufaransa), Wilfried Zaha (Crystal Palace, England), Jérémie Boga (Grenada/Uhispania), Salomon Kalou (Hertha Berlin, Ujerumani), Seydou Doumbia (FC Bâsel, Uswizi)
No comments