Kumbe Haji Mwinyi aliitosa Simba!
Zanzibar. Baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kucheza Yanga, mlinzi wa kushoto Mwinyi Haji Ngwali “Bagawai” ametoboa siri iliyomfanya kubakia Jangwani licha ya kupokea ofa ya Simba.
Mwinyi amekiri kuongeza mkataba wa miaka miwili Yanga na pia aliweka wazi kuwa Simba walihitaji huduma yake lakini hakuweza kufanya hivyo.
“Nimeongeza mkataba wa miaka miwili Yanga, licha ya kwamba Simba walinihitaji na mazungumzo yalikuwa yameshaanza na yamefikia pazuri," alisema Haji.
Mwinyi alijiunga na Yanga miaka miwili iliyopita akitokea KMKM ya Zanzibar na katika kipindi hicho ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu na klabu hiyo.
No comments