Ads

Dembele atamani kusajiliwa Barcelona...



Image result for dembele dortmund

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele amesema tangu mwaka jana alikuwa akiwasilina na Barcelona ambao hivi sasa wameonyesha nia kuwa wanamhitaji.
Barcelona wamekuwa kwenye mbio za kumuwania mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya  ushambuliaji msimu ujao.
Dembele mwenye miaka 20 alifanikiwa kuifungia Ufaransa bao dakika ya 78 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya England, mechi iliyochezwa jijini Paris.
Ufaransa waliibuka na ushindi wa mbao 3-2. Nyota huyo wa Dortmund imeripotiwa amevutiwa na ofa ya Barcelona, hata hivyo ana mkataba na Dortmund hadi mwaka 2021. 
Dembele aliingia kukipiga Bundesliga akitokea Rennes mwaka uliopita. Hata hivyo, Barcelona imesema bado inafuatilia uwezekano wa kumnyakua mchezaji huyo.
Dembele amecheza mechi 32 za Bundesliga akiwa na Dortmund msimu wa 2016-17, huku akifunga mabao sita.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.