Ads

SIASAMambo manne aliyozungumza Maalim Seif kuhusu Lowassa na Lipumba...........



Siasa

Leo May 3 2017 kupitia Clouds 360 ya Clouds TV Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi ‘CUF’, Maalim Seif Sharifu Hamadi amezungumzia kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya CUF na mustakabali wa chama hicho.
Aidha, katika kuuzungumzia mgogoro huo, pia Maalim Seif aligusia kuhusu Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa kujiunga na UKUWA kitendo kilichopelekea Prof. Lipumba kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa CUF akisema kuwa Prof. Lipumba alikuwa mmoja wa watu waliomkaribisha Lowassa kujiunga na UKAWA kwa kuwashawishi viongozi wa Muungano huo wampokee na kupendekeza jina la muungano huo.
Awali, Maalim Seif alisema kuwa Lipumba ndiye aliasisi jina la UKAWA akisema: “Prof. Lipumba ndio alitoa jina la UKAWA.
Kisha baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa kukatwa jina lake katika kugombea Urais kupitia CCM alikaribishwa UKAWA na Prof. Lipumba akisema: “Baada ya Lowassa kukatwa na CCM, Prof. Lipumba ndio alimkaribisha UKAWA na kuwashawishi viongozi wa UKAWA wampokee.
Na alipoulizwa kuhusu kujiuzulu kwa Prof. Lipumba kisha kurudia tena katika wadhifa wake ndani ya CUF, Maalim Seif alisema: “Prof. Lipumba alijiuzulu, na Katiba ya CUF hairuhusu kitendo cha ‘kutengua’ kujiuzulu kwake.
Aidha, Makamu huyo wa Kwanza wa Serikali iliyopita ya Mapinduzi Zanzibar aliongeza kwa kusema kuwa Prof. Lipumba na kundi lake wanafanya uhalifu kuzikalia Ofisi za CUF: “Prof. Lipumba na kundi lake ambao wamekalia Ofisi za CUF, sio wanachama wa CUF na hivyo wanafanya uhalifu kukalia Ofisi hizo.” – Maalim Seif.
VIDEO: Ziara ya Maalim Seif Jijini Dar es Salaam May 2 2017

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.