Katika kipindi cha #Clouds360 kinachoendelea muda huu, msanii #RomaMkatoliki ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Mh Kessy ( Mbunge wa Jimbo la Nkasi ) kutaja jina lake Bungeni na kudai kwamba Roma aliimba wimbo kumhusu Rais. Hivi karibuni Mh Kessy aliongelea ' sakata la kutekwa kwa Roma ' na kudai kwamba hayo yalitokea baada ya Roma kuimba wimbo unaomkashifu Rais.
.
.
#RomaMkatoliki ameeleza kwamba alisikitishwa na kitendo hicho kwani Mbunge huyo alichokisema kilikuwa kitu cha uongo. " Tena alitaha kabisa jina langu. Akitoka nje ya Bunge yule ukimuuliza hana uhakika. Lakini ameongea vile kwa sababu yeye ana mahali pa kusemea. Je mimi mimi nitasemea wapi ? " - #RomaMkatoliki
No comments