Ads

Mwanahabari mfichuzi wa mihadarati auwawa Mexico........

Javier Valdez ameripoti pakubwa dhidi ya magenge ya ulanguzi wa mihadarati Mexico


Haki miliki ya picha

Mwaandishi habari aliyeshinda matuzo mengi kuhusiana na taarifa zake nyingi ya ufichuzi wa shughuli za makundi, yanayojihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico, ameuwawa.
Javier Valdez, aliuwawa na watu wenye silaha ambao walimiminia gari lake risasi akiwa katika mji wa Culiacán- jimbo la Sinaloa, kaskazini mwa nchi hiyo.
Javier Valdez aliuwawa alipokuwa akiliendesha gari lake kwenda ofisini kuliko na mtandao wake wa habari alilolianzisha huko Rio Doce.
Pia aliifanyia kazi shirika la habari la AFP, na gazeti moja maarufu nchini Mexico- La Jornada.
Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, ameamuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na kile alichosema uhalifu wa kutisha.
AFP nayo inasema kuwa Bwana Valdez alikuwa ameonyesha utendaki wa hali ya juu ya upekuzi dhidi ya walanguzi wa mihadarati, licha ya kufahamu kuwa alikuwa anahatarisha maisha yake.
Waandishi wanne wameuwawa nchini Mexico, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.