BARABARA ya Mwenge Hadi Morocco Ilojengwa kwa Fedha za Uhuru Yaanza Kuharibika...............
Rais Magufuli aliamuru Sh bilioni 4 zilizopaswa kutumika kugharamia sherehe za sikukuu ya Uhuru, ambazo zingefanyika Desemba 9, 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco yenye Kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami. Kazi lifanyika mara tu tangazo kutoka, inasemekana hata tenda haikutangazwa. Bali Mkandalasi aliingia site mara moja na kuanza kutengeneza.
Leo nlipofika Dar es Salaam Mwaka mmoja baada ya Ujenzi, Nimeshangaa Kukuta barabara ina mawimbi na imeanza kuharibika. Nmesikitika sana sema sina la kufanya.
Nlitegemea kwa kuwa ilikuwa ndo barabara yake ya Kwanza tangu awe Rais basi ingekuwa ya kiwango cha juu na Mfano kwa barabara nyingine. Kwanza alama za barabara hazieleweki. Na ndicho kilinifanya nianze kuikagua. Au bado haijakabidhiwa? Kama bado isipokelewe.
Katika Barabara za Dar es Salaam ni barabara moja tu ya Sam Nujoma ambayo nimeona angalau inakidhi haja. Naomba Rais Magufuli aendelee kutumbua Majipu hadi nchi ikae sawa. Hivi walitaka rais Magufuli ndo aingie site kusimamia Ujenzi wa barabara?
Tumechoka ubabaishaji.
No comments