Sikutaka watu wajue nina mimba
Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Bingwa huyo wa taji la Grand slam mara 23 alichapisha picha katika mtandao huo wa kijamii akijiangalia katika kioo akiwa ameandika ujumbe wiki 20 kabla ya kufuta kabla ya wasimamizi wake kuthibitisha habari hizo.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.
''Nilikuwa nikijihifadhia'', alisema.
''Nilikuwa nikiendelea vizuri lakini bahati mbaya picha moja nikaichapisha katika Snapchat''.
Bingwa huyo nambari moja kwa upande wa wanawake anatarajiwa kujifungua majira ya vuli, akisema kua aligundua kwamba ana mimba siku mbili kabla ya mashindano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Raia huyo wa Marekani alimshinda dadake Venus katika fainali na kuimarisha rekodi yake ya mataji 23 ya Grand Slam.
''haikuwa rahisi'',alisema. Unasikia habari kuhusu walio na mimba, wanakuwa wagonjwa, na wanachoka''.
''Niwe na mimba au la nilijua kwamba ni lazima nishinde. Kila mara ninapocheza, ninatarajiwa kushinda. Iwapo sishindi zinakuwa habari kubwa zaidi''.
No comments