Ads

Serengeti Boys yaichapa Cameroon...................

serengeti


Haki miliki ya picha

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' imepata ushindi wa tatu mfululizo katika mechi za kimataifa katika maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 yatakayoanza mwezi Mei 14, 2017.
Serengeti Boys wameifunga timu ya taifa ya vijana ya Cameroon kwa goli 1-0 ,goli lililofungwa na Ally Ng'anzi kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Huu ni mchezo wa tatu Serengeti inashinda mfululizo, ilishinda mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon zilizochezwa nchini Morocco ambako Serengeti ilikua imeweka kambi kabla ya kwenda Cameroon.
Baada ya kumaliza kambi nchini Cameroon itaondoka na kuelekea Gabon ambako zitafanyika fainali za michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa nane.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.