Home
/
KIMA\TAIFA
/
MAREKANI Yaweka Mtambo Kuilinda Korea Kusini Dhidi ya Makombora ya Korea Kaskazini..!!
MAREKANI Yaweka Mtambo Kuilinda Korea Kusini Dhidi ya Makombora ya Korea Kaskazini..!!
Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.
Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora ambao hufahamika kitaalamu kama Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unasimikwa kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora yake.
Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa na kuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mtambo huo unajengwa katika Wilaya ya Seongju lakini China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.
No comments