Hisia kali zatolewa kuhusu filamu mpya ya Bruce Lee
Filamu hiyo 'Birth of the Dragon' inaonyesha maisha ya nyota huyo alipokuwa mdogo nchini Marekani pamoja na pigano lake lililozua utata dhidi ya bwana Wong Jack Man mwaka 1964.
Filamu hiyo ilioelekezwa na George Nolfi ,ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika sherehe ya filamu ya Toronto.
Lakini mashabiki wengi wamepinga vile inavyomuonyesha Bruce Lee,wakisema kuwa nyota huyo alishushwa sana hadhi yake katika filamu inayozungmzia maisha yake yeye mwenyewe.
''Huu ni utani? Nilikuwa hapa umuona Bruce Lee,lakini wakati mwingi wamekuwa wakimuonya mtu mmoja mweupe'',aliandika mtumiaji wa IMDb ticklegear katika shambulio la mtanda wa kijamii.
"Badala ya kusherehekea vile Bruce Lee alivyokuwa mnyama ,wamemfanya aonekane mtu muoga na mwenye wivu.Hii ni sawa na kushusha hadhi ya muigizaji huyo badala ya kuonyesha maisha yake''.
Aliongezea: Ni filamu mbaya ,nisingeipendelea kwa sababu inaharibu historia ya Bruce Lee kwa kuongeza uongo mwingi.
No comments