HALI TETE KWA WANANCHI WA VINGUNGUTI........
Wananchi wa maeneo ya Vingunguti wilaya ya Ilala wachoshwa na hali ya mazingira wanayoishi na kuamua kuiomba serikali msaada.Wakiongea na 24 hours blog baadhi ya wakazi wanaokaa pembezoni mwa reli inayofanya usafiri wa treni zake kutoka Dar es salaam kwenda kigoma wamesema kuwa nikweli Serikali inajitahidi kusisitiza swala la usafi lakini bado kwa maeneo yao hali ni tete.
Wamesema kuwa mitaro inayopita pembezoni mwa reli hiyo halikadhalika kwenye baadhi ya nyumba wanazoishi imekuwa ikihifadhi maji machafu ambayo yamekuwa yakileta madhara ya kiafya kwa watoto pia kwa watu wazima. wamesema chanzo cha maji hayo ni moja baa iliyopo maeneo hayo kwani imekuwa ikimwaga uchafu wake nakufanya kutuama mkwakipindi kikubwa sasa.
Picha na ally mshana
No comments