Diamond Platnumz na Mohombi Kuja na Kolabo
Tuzo za MTV MAMA huwakutanisha wasanii wengi wa Afrika kwa wakati mmoja. Si kila anayehudhuria huwa ametajwa kuwania tuzo, bali wengine huenda kwaajili ya kutafuta connection.
Na wengine hutumia fursa hiyo kwenda kufanya video na wasanii waliowashirikisha ili kupunguza gharama za kuwasafirisha kuwapeleka SA kwaajili hiyo. Miongoni mwa watu waliotumia fursa hiyo ni rapper wa Malawi, Tay Grin aliyewahi kuweka wazi nia yake ya kutaka kufanya kazi na Diamond.
Na sasa huenda hilo limekamilika baada ya kuungana na muimbaji huyo wa ‘Salome’ jijini Johannesburg kufanya video ya wimbo unaonekana amemshirikisha Diamond pamoja na msanii wa Sweden, Mohombi.
“We out here with the boy @diamondplatnumz video shoot,” ameandika Tay Grin kwenye picha hiyo ya juu aliyoiweka Instagram. “It’s fire trust! With @mohombimusic ( I wanna boom bang bang with your body ) @iamlumino @chronicles_of_karim_cazal colin the “boss” it’s all love out here! Great things in the pipeline.”
Naye Mohombi aliweka picha akiwa na Diamond kwenye mtandao huo na kuandika: Big Things Coming !!!! #AfricaUnite with my bro @diamondplatnumz
No comments