Ads

Diamond Awajibu Wabaya Wake Kwa Njia Hii.............



Ijumaa hii Diamond Platnumz ameachia verse ya pili ya remix ya wimbo wa ‘All the way up’ wa Fat Joe & Remy Ma huku akioekana kuwa jibu wanaomfuatilia kwenye anga zake huku pia mashairi hayo yakidaiwa kuwalenga baadhi ya wasanii wenzake kwenye mistari hiyo.

Hivi karibuni mwimbaji huyo alidaiwa kuwa anatoka na model wa kwenye video yake mpya ya Salome, Hamisa Mobetto kitu ambacho muimbaji huyo hajawahi kukiongelea lakini kupitia wimbo huo amepigilia msumari kwenye mifupa ya wabaya wake. “Mara nakula Hamisa Mobetto, eti Sepenga kaja magheto, ilimradi Zari apate mchecheto, Tale waambie waache unambinambi hata nikila wote dini yangu sio zambi,” amerap Diamond kwenye wimbo huo.

Mstari mwingine unaodaiwa kuleta utata ni ule unaosema, “Siachi pengo hadi waombe poo, wao wakipost tembo si tunapost show.” Sikiliza wimbo huo hapa chini.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.