Ads

JULIO KATANGAZA SABABU ZA KUSTAAFU KUFUNDISHA SOKA.......

Image result for julio kocha wa mwadui
Jamhuri Kihwelu 'Julio'-Kocha Mwadui FC
Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ataamua kustaafu kufundisha soka endapo baadhi ya matukio yataendelea kujitokeza katika ligi kuu ya Tanzania bara.
“Nafikiri Julio nikitoka, akatokea mtu mwingine akatoka, halafu wakatoka wengine wote ambao hawapendi upuuzi nadhani tutaendelea, ni jambo la aibu”, alisema Julio wakati akizungumza kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Tumekuwa wa tano kwenye riadha za marathoni Olympic Rio, tunashangilia mtu aliyekuwa watano, ni jambo zuri  kwetu Tanzania kwasababu hatujazoea kufanya vizuri. Simbezi aliyekuwa watano, amefanya kazi nzuri kwasababu marathoni wanakimbia watu wengi. Ukija kwenye boxing siku zote tunapigwa na tukishika nafasi ya tano tunashangilia.”
“Leo tunashangilia Uganda kwenda kuicheza AFCON badala ya kushangilia timu yetu, hii inatokana na malezi ambayo tunakuwa nayo, tumekuwa na mazoea ambayo yamejenga tabia kwahiyo ili tujifunze lazima tufanye kazi kwa uadilifu ili tufike kwenye kilele cha mafanikio.”
Alipoulizwa kama kweli ataachana na soka endapo mambo hayatabadilika, Julio alisema: “Nitaita waandishi wa habari halafu nitachukua vyeti vyang na kuvining’iniza ukutani ili ibaki kumbukumbu kwa wanangu na wajuu kwamba babu yetu alikuwa kocha.”
“Juzi tumefungwa goli moja na Nigeria, magazeti yameandika Nigeria wamelala na viatu wakati huo wametufunga goli moja, inasaidia nini Nigeria kulala na viatu. Mimi nilitarajia baada ya kupoteza kichwa cha habari kama hiki kinatusaidia nini?”
“Mitaka kuona kama mpira wetu unaenda hovyo, Kim Polsen alikuwa kocha wa timu ya taifa na alikuwa na mipango ya kwenda AFCON mwaka 2017 lakini akafukuzwa leo amerudishwa kwenye timu za taifa za vijana, Serengeti Boys inafanya maajabu, kwanini wasingemwacha kipindi kile lakini sasahivi wamemrudisha kwa lipi zuri alilofanya na tayari alishaonekana mbaya?”

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.