Uchumi wa taifa la Nigeria waporomoka........
Takwimu zilizotolewa kuhusu pato la ndani la taifa (GDP)zinaonyesha kuwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika kilishuka kwa zaidi ya asilimia 2% katika robo ya pili ya mwaka huu.
Hasara hii ya kiuchumi si jambo lililowashtua mamilioni ya raia wa Nigeria.
Wengi wanasema hawajawahi kushuhudia ugumu wa maisha kama walio nao sasa.
Kushuka kwa bei za mafuta duniani kumeiathiri Nigeria vibaya
Serikali hutegemea mauzo ya mafuta kwa takriban asimilia 70% yamapato yake.
Lakini wakosoaji wanasema sera ya serikali imeifanya hali kuwa hata mbaya zaidi.
Uamuzi wa kuchelewa kutathmini upya thamani ya sarafu ya Nigeria ina maanisha kuwa biashara nyingi zitakwama kutokana na ugumu wa kupata dola kwa ajili yamalipo ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje suala ambalo linaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi mzima wa taifa.
Kutoka na shinikizo lisilofahamika serikali ilibadili mbinu zake na kuifanya thamani ya sarafu ya taifa hilo Naira kuporomoka.
Hiyo ilisababisha kupata kwa hasara ya taifa , lakini matumaini yalikuwa ni kuwavutia wawekezaji na hivyo kuinua uchumi.
Serikali pia inasema taifa linahitaji kuwa na mauzo ya nje machache. Inataka kuona uzalishaji zaidi wa ndani ya taifa.
BBC Swahili
No comments