Ads

NAPE AVIFUNDISHA KAZI VYOMBO VYA HABARI.......


Yatosha

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ipo haja kwa vyombo vya habari vya Afrika kuandika habari zilizo njema zinazohusu bara hilo na taarifa hizo zifikie nchi za magharibi ili nchi hizo ziwe na maono chanya juu ya Afrika.

Alisema hivyo  Dar es Salaam wakati alipozungumza kwenye kongamano la kidiplomasia kati ya China na Afrika.nape nnnauyeAlisema suala hilo ni changamoto kubwa kwa vyombo vya habari kwani mara nyingi vimekuwa vikiandika kama hakuna jambo jema katika bara la Afrika.

“Vyombo vya habari viandike yale yaliyo mema ya Afrika na kuhakikisha taarifa hizo zinazungumzwa duniani, wenzetu wamekuwa wakitumia vyombo vyao kuandika taarifa chanya za nchi zao,” alisema Nape.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.