Ads

JPM ATATUMBUA JIPU MWANZA LEO?


RAIS John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humu leo, ambapo atakagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, Rais Magufuli atawasili Mwanza leo asubuhi akitokea Geita ambako alikuwa kwenye mapumziko wilayani Chato.MAGUFULI NA JANETH“Rais anatarajiwa kuwasili hapa kesho (leo) akitokea mkoani Geita, ataanzia ziara yake ya kikazi wilayani Sengerema, ambako pia atapata fursa ya kuzungumza na wananchi juu ya mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitekelezwa na serikali,” alisema Mongella.

Alisema baadaye atarejea jijini Mwanza ambako akiwa njiani atakuwa anasimama kuzungumza na kusalimiana na wananchi kulingana na ratiba itakavyokuwa inaruhusu na atawasili jijini Mwanza kwa mapumziko.

Alisema kesho Rais Magufuli atapata fursa ya kutembelea miradi ya ujenzi wa barabara ya Mwanza- Airport pamoja na kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu ambako ataweka jiwe la msingi katika daraja hilo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.