Ads

SHTUKIZA YA MAJALIWA YAFICHUA UFISADI WA BILIONI 10 MBEYA.......


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kuwepo kwa ubadhilifu katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa.

“Inasikitisha ujenzi wa soko hili kuingia ubabaishaji. Ujenzi wa soko ungegharimu sh bilioni 16 ila sasa watendaji wamefanya mambo ya hovyo na kufikia sh bilioni 26 hatuwezi kuwavumilia lazima hatua zichukuliwe kwa wote watakaobainika katika ubadhilifu huu,” alisema.wAZIRI mKUU mWANJELWAPia amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kufanya uchunguzi na kubaini nani aliyetafuna sh milioni 489 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya uendelezaji wa soko hilo ambazo hazijulikani zilipo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo  wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko la Mwanjelwa na kubaini ubadhilifu wa fedha katika ujenzi wa soko hilo.

Waziri Mkuu amesema mara baada ya CAG kumaliza kufanya ukaguzi atatoa taarifa na mtu yeyote atakayetajwa katika ripoti hiyo kuwa amehusika na ubadhilifu huo atawajibika hata kama yuko nje ya Jiji la Mbeya.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.