Ads

Neyonzima na Busungu kazi hawana tena yanga........

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amewafungia kazi wachezaji Haruna Niyonzima na Malimi Busungu kwa kuwapa mazoezi maalumu kwa ajili ya kuwakabili MO Bejaia ya Algeria.

Yanga itacheza na MO Bejaia mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika huku wenyeji wakisaka ushindi wa kwanza baada ya kupoteza mechi tatu na kutoka sare mchezo mmoja.

Katika mazoezi ya jana asubuhi, kocha Pluijm alionekana akiwazidishia dozi wachezaji hao wawili kwa kuwapa mazoezi magumu huku wachezaji wengine wakifundishwa na kocha msaidizi Juma Mwambusi.Niyonzima-HarunaMshambuliaji Donald Ngoma ataukosa mchezo huo wa Jumamosi kutokana na kuwa na kadi mbili za njano na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Busungu na Niyonzima anatarajiwa kuanza kwenye eneo la kiungo baada ya mchezo uliopita dhidi ya Medeama ya Ghana kuanzia benchi.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.