Ads

YANGA MKOTAYARI KUMPOKEA CHANONGO...


WINGA wa zamani wa Simba, Haruna Chanongo, huenda akasaini Yanga muda wowote wikiendi hii huku Simon Msuva wa Jangwani akitajwa kuwaniwa na timu za Arabuni.
Tayari Yanga imeshawapa mikataba Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe, pia imemsajili, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ na Ibrahim Ajibu ambaye bado hajawekwa wazi.
Chanongo mwenye uwezo wa kutumia miguu yote miwili, lakini mzuri zaidi anapocheza winga ya kulia, anatua Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani ambayo haikumbuki hata lini mara ya mwisho kuongoza Ligi Kuu Bara.
Habari za ndani zinadai kwamba kuna mambo machache sana baina ya dogo tu ambayo yanakwamisha usajili wake, lakini alitakiwa kusaini mapema mwanzoni mwa wiki hii.
Mwanaspoti ilimtafuta mchezaji mwenyewe ambaye alisema: “Kama jambo hilo lipo basi ukifika wakati wake mtajua tu, mimi sina maneno mengi.”

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.