Ads

PRISON WAGOMA KUUZA MCHEZAJI WAO YEYOTO...


Image result for yanga na prison mbeya

Uongozi mpya Prisons umegoma kuwaachia nyota wake wanaotakiwa na klabu nyingine.
Taarifa za uhakika kutoka klabu hiyo zinadai kuwa mabeki  beki Salum Kimenya anawaniwa na Azam, James Mwasote ,Nurdin Chona wakihitajika na  klabu ya Simba huku mshambuliaji  Victor Hangaya aking’ang’aniwa na Mbeya City.
Katibu Mkuu wa Prisons, Havintishi Abdallah, alisema taarifa hizo wamezipata na tayari wamekaa na wachezaji hao wanaotajwa kuihama klabu hiyo.
Alisema wanajua soka ni biashara kwa wachezaji na lazima wataihama klabu hiyo, lakini watahama pale watakapopatikana wakuziba mapengo ndipo wanaweza kuwaachia kwenda kusaini klabu zingine.
‘’Tuliambiwa Kimenya amesaini Azam kwa miaka miwili pamoja na wengine ambao ilisemekana wapo kwenye mazungumzo na timu hizo, lakini kwa vyovyote vile na sisi hatuwezi kuruhusu roho ya timu inyofoke kizembe namna hiyo.’’
Aliongeza ‘’Kimenya ni mwajiriwa wa jeshi la Magereza, lakini hata hao ambao siyo waajiriwa tukiona wanaisaidia timu hatutaruhusu kuwaachia hivi hivi, bora tukae nao ili tujue tatizo nini hasa,’’alisema Abdallah.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.