Ads

Smalling amvaa Mourinho....



Image result for smaling
London, England. Chris Smalling amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake,  hana namna nyingine ya kumfurahisha kocha wake, Jose Mourinho.
Tangu msimu ulioisha, Mourinho alionekana kumsakama mchezaji huo wakati Swansea City ilipoonyesha nia ya kumtaka.
Smalling alisema hawezi kucheza kutokana na kukabiliwa na maumivu makali pamoja na matatizo ya kuchanika ulimi.
Kocho huyo alionekana kuwakera Smalling na Philip Jones baada ya kuwahimiza kwamba wajitahidi kurudi kwenye hali ya kawaida kutokana na kuwa na majeraha yao ya muda mrefu.
Hata hivyo, Smalling hakupendezewa na kauli ya Mourinho lakini akasema inaonyesha kocha huyo alikuwa anajaribu kuonyesha hasira zake kwenye jambo ambalo ni la kitaalamu.
Mchezaji huyo alimtaka Mourinho aombe radhi kwa kauli yake aliyoitoa kwani kuumia kwake na kupumzika ni suala la kitaalamu.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.