nchi inayoongoza kwa Wajawazito kunywa Pombe....
Mtandao maarufu wa Daily Mail uliripoti kuwa wanawake wengi nchini Uingereza hunywa pombe wakati wa ujauzito kuliko wanawake wote wa Ulaya wakikadiriwa kunywa kufikia hadi kiwango cha uniti mbili kwa wiki.
Watafiti wamebaini kuwa 28.5% ya wanawake kutoka Uingereza wanakunywa sana pombe licha ya kujua kuwa wana ujauzito wakifuatiwa na wajawazito wa Urusi ambao wana 26.5% huku Sweden ikiwa ya pili kutoka chini ikiwa na 7.2% ikifuatiwa na Norway ambayo ni ya mwisho kwenye list ikiwa na 4.1%.
Watafiti nchini Norway waliwatafiti wanawake wajawazito 7,905 kutoka nchi 11 za Ulaya na kubaini kuwa wanawake wanaotumia ulevi wakati wa ujauzito ni watu wazima, walioelimika sana na waliokuwa kwenye ajira. Utafiti huo ulifanywa katika nchi za Croatia, Finland, Ufaransa, Italia, Norway, Poland, Urusi, Serbia, Sweden, Switzerland na Uingereza.
Mwandishi wa utafiti huo Professor Hedvig Nordeng, alisema: “Tofauti katika tabia za unywaji pombe kwa wajawazito baina ya nchi hizi unaweza kuwa na maelezo mengi. Kunaweza kuwa na tofauti katika miongozo ya Taifa au kampeni za elimu kuhusu kunywa wakati wa ujauzito, tofauti za kutunza ujauzito na mtazamo juu ya matumizi ya ulevi wakati wa ujauzito, au mjumuiko wa mambo yote haya.”
Chanzo millard Ayo
No comments