Msiba wa Ivan Wamuibua Baba Yake Zari..Afunguka Haya Mazito...
Kwa muda mrefu staa wa muziki na mjasiriamali wa Afrika Mashariki, raia wa nchini Uganda, mwenye maskani yake mengine huko Pretoria, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amekuwa akionekana Bongo na mama yake mzazi, Halima Hassan hivyo kuibua sintofahamu juu ya alipo baba yake, Hassan Tiale.
Hata hivyo, kifo cha mkwe wake yaani aliyekuwa mume wa mwanaye, Zari, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, kimemaliza utata huo baada ya kumuibua mzee huyo aliyekuwa amejaa tele kwenye msiba huo nchini Uganda. Mzee Hassan alikuwa mmoja wa watu lukuki waliohuzunishwa na kifo cha Ivan ambapo alisema kuwa, alilazimika kuacha shughuli zake ili kuhudhuria msiba huo kwa namna alivyokuwa akiivana na Ivan. “Msiba huu umenigusa sana. Nilipigiwa simu nikiwa Nairobi (Kenya) ambako nilikwenda kumuozesha kijana wangu bibi (mke).
“Nilisikia Ivan aliteleza kwa ajili ya presha, akaanguka chini, akachukuliwa, akapelekwa hospitalini Afrika Kusini, akawekwa ICU (chumba cha wagonjwa mahututi). “Niliendelea kupigiwa simu nyingi, nikaambiwa hali inazidi kuwa mbaya. Niliambiwa mshipa wa kupeleka damu kwenye ubongo ulipasuka. Hadi zilipopita saa ishirini na nne na kuendelea ndiyo niliambiwa amefariki dunia.
“ B a s i , n d i y o nikaacha shughuli z a n g u nikaja hapa (nyumbani kwa Ivan, Kampala) k w e n y e m s i b a maana alikuwa mtu mzuri sana. Hayo mengine ni manenomaneno ambayo ya nasemwa.
“Kwa kweli Ivan alikuwa mtu mzuri sana na ndiyo maana kila mtu anamzungumzia vizuri,” alikaririwa mzee huyo.
Naye dada wa Zari aliyejitambulisha kwa jina la Madina Hassan alisema kuwa, alifahamiana na Ivan alipofika nyumbani kwao kujitambulisha wakati Zari alipopata mtoto wao wa kwanza wa kiume, Pinto.
“Nilishtushwa sana na kifo chake kwa sababu alikuwa mtu aliyependa kufurahi wakati wote, hivyo ni pigo kubwa kwangu,” alisema Madina. Ivan aliyezaa watoto watatu wa kiume na Zari kabla ya kutengana alizikwa Mei 30, mwaka huu kijijini kwao, Nakalilo nchini Uganda.
No comments