Mtandao wa England uliyoripoti kuhusu SportPesa Super Cup...............
Najua inawezekana ukawa na shauku ya kuona michuano ya SportPesa Super Cup inafanyika mapema zaidi kutokana na upendo wako na soka baada ya kusikia kuwa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sport Pesa imeanzisha mashindano hayo na yataanza June 5 hadi June 11 2017.
Good news nyingine iliyoritipotiwa leo na moja kati ya mitandao mikubwa England ni kuhusiana na club ya Everton kuwa itakuja Tanzania na Alhamisi ya July 13 itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na moja kati ya timu nane zitakazoshiriki michuano ya SportPesa Super Cup.
Mtandao wa liverpoolecho.co.uk ndio umeripoti taarifa hizi huku ikithibitisha kuwa timu za Simba, Yanga, Singida United, Jang’ombe Boys, AFC Leopards, Tusker FC, Gor Mahia na Nakuru All Stars ndio zitashiriki michuano hiyo na moja kati ya timu hizo itacheza na Everton.
Game ya Everton itakuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ujio wao Tanzania ni sehemu yao ya makubaliano yao ya udhamini na SportPesa, mtandao waliverpoolecho.co.uk ni moja kati ya mitandao mikubwa katika jiji la Liverpool ambapo inatokea timu ya Everton.
No comments