Ads

FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP...............


Image may contain: text

Kesho Jumamosi, Mei 27 mwaka huu Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zitakutana Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup - ASFC 2016/17 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

Kwa mujibu wa kanuni ya 7 (2) za michuano ya ASFC, ratiba ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD itatolewa na TFF na ndiyo kesho itachezwa.

Kadhalika kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (2), Mshindi wa mchezo wa fainali (Kwa msimu huu kati ya Simba na Mbao), ndiye akayekuwa Bingwa wa Kombe la ASFC - HD, atapewa Kombe la Ubingwa na zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni hamisini (50,000,000/-) kama zilivyoainishwa kwenye waraka wa zawadi wa michuano.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.