Kumbe utovu wa nidhamu kwa wachezaji ndiyo chanzo cha kushuka kwa thamani ya soka la hapa Tanzania......
Hivyo ndivyo mambo yalivyo
Sikuzote zote mkubwa hakanywi lakini
huelekezwa ili ajirekebishe, na hivi ndivyo ilivyo kwa timu za wenzetu huko
ulaya.Ambapo imeonekana kuwa nidhamu ya
wachezaji uwanjani ndiyo inazifanya timu na ligi za ulaya kuonekana bora
ulimenguni.
Imeonekana kuwa kwa wachezaji wa
timu za huko majuu(ulaya) wamekuwa wakionyesha nidhamu kwa kipindi chote wakiwa na makocha wao uwanjani, mazoezini
na hata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo tofauti na baadhi ya wachezaji wa
hapa Tanzania.Baadhi ya wachezaji wameonekana kutokuwa na nidhamu hasa
wanapokuwa uwanjani nahii kupelekea sifa mbaya kwa ligi za mpira hapa nchini.
Akizungumza na 24
hours blog moja kati ya mdau wa
mpira hapa Tanzania Bw Mussa Ramadhani maarufu kwa jina la Ramso The Blues ambaye ni shabiki wa timu ya Chelsea ya huko
uingereza alisema kuwa, amekuwa shabiki wa timu hiyo(Chelsea)kwa muda mrefu
sana na hivyo kugundua kuwa timu zinazoshiriki ligi ya uingereza(EPL) ikiwemo
Chelsea wachezaji wake wana nidhamu ya hali ya juu na hicho ndicho kinacho
ifanya ligi hiyo kukubalika ulimwenguni.
Mussa alifunguka nakuelezea
kuwa, kwa Tanzania iko tofauti kabisa kwani mchezaji anaweza kuvunja sheria za
soka(mpira) na kuamua kufanya chochote anachojiskia.Kwa mfano mchezaji anaweza
kumpiga refa uwanjani hii yote nikukosa nidhamu na pia mchezaji anapoeleweshwa
kwa kosa alilolifanya hujiona yeye yupo sahihi na kusimamia upande wake.Lakini kitendo
hiki ndo chanzo cha kuharibu mpira wa hapa Tanzania na pia kushuka kiwango kwa
wachezaji.
Mussa aliongezea kuwa, licha ya
nidhamu wachezaji wa timu za huko majuu huwa wanacheza mpira kwa jitihada zote
kwa kuwa wanajua ndiyo ajira(kazi) yao tofauti na wachezaji wa hapa Tanzania
wanacheza mpira ili kuonekana na sio kuwa wanacheza kama kazi na hiki kinachowafanya wenzetu kuwa juu.
“kiujumla wachezaji wa timu za
huko majuu wana nidhamu lakini licha ya nidhamu huwa wanacheza mpira kwa
jitihada zote kwa kuwa wanajua ndiyo kazi yao.Tofati na wachezaji wa hapa
Tanzania wanacheza mpira ili kuonekana na sio kuwa wanacheza mpira kama sehemu
ya kazi na hiki kinawafanya wenzetu kuwa
juu siku zote” Moja kati ya mashabiki wa timu ya Chelsea hapa Tanzania Bw mussa
Ramadhani alisema;
Yapo matukio ambayo yanatendeka
ndani ya uwanja yasiyo yakinidhamu nahii ni kwenye michezo mbalimbali ya ligi
kuu Tanzania bara(VPL) halikadhalika michuano mingine lakini kutokana na
uongozi(TFF) kutofuatilia kwakina matukio haya ndo mana mara nyingi huwa
yanajirudia.
January 2016 mchezaji Juma Nyoso(Mbeya
City) alifanya kitendo kisicho cha nidhamu
kumzalilisha mchezaji mwenzake wa timu ya Azam John Bokko na uongozi ulichukuchukua uamuzi wa kumfungia kutocheza
mpira(mechi) hata moja mwaka mzima wa 2016.
24 hours blog imeandaliwa
na ally mshana
No comments